Yanga kufanya uchaguzi wa nafasi zote

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Mar 2019
Yanga kufanya uchaguzi wa nafasi zote

Baada ya kikao cha Baraza la Wadhamini la klabu ya Yanga na Kamati ya Utendaji ya Yanga, viongozi hao wamefikia makubaliano ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo wakiachana na mpango wa kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la Yanga Mh George Mkuchika amesema kutokana na idadi kubwa ya viongozi wa Yanga kuwa wamejiuzulu, wameonelea ni vyema ukafanyika uchaguzi Mkuu wa kuwapata viongozi wapya, uchaguzi ambao ulipaswa kufanyika mwakani kwa mujibu wa Katiba ya Yanga

"Badala ya kufanya Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa kuziba mapengo, tumekubaliana kwa kauli moja, Baraza la Wadhamini, Kamati ya Utendaji na wenzetu wa kanda mkoa wa Dar es salaam, tumekubaliana tufanye Mkutano Mkuu wa Uchaguzi mwaka huu," amesema Mkuchika

Nae Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Samwel Lukumay amesema viongozi wa timu hiyo wamekubaliana na Baraza la Wadhamini juu ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa kuwapata viongozi wapya mwaka huu badala ya mwakani.

Amesema ni kweli viongozi wengi wameachia ngazi, pia mwakani kutakuwa na uchaguzi Mkuu wa Serikali, hivyo ni vyema badala ya kufanya uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi zilizowazi halafu mwakani kufanya tena uchaguzi Mkuu, ni vyema uchaguzi huo ukafanyika mwaka huu

Lukumay amesema wataitisha Mkutano Mkuu wa Wanachama wa klabu ya Yanga hivi karibuni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’