Msafara wa wachezaji 20 wa kikosi cha Yanga na viongozi nane wa benchi la ufundi unatarajiwa kuondoka kesho Alhamisi asubuhi kuelekea mkoani Iringa tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Lipuli Fc
Mchezo huo utapigwa siku ya Jumamosi, March 16 2019 kwenye uwanja wa Samora
Msemaji wa klabu ya Yanga Dismas Ten amesema morali ya wachezaji walioandaliwa kwa ajili ya mchezo huo iko juu na wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mchezo huo
Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 67, itakuwa ikisaka alama tatu muhimu ili kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kufikisha alama 70 msimu huu
ADVERTISE HERE