Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Yanga kesho wanatarajiwa kuelekea mkoani Iringa kuifuata Lipuli Fc tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Samora Jumamosi, March 16 2019
Yanga inakwenda mkoani Iringa ikiwa na matumaini makubwa ya kuendeleza wimbi la ushindi na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga Noel Mwandila amesema wanafahamu kuna changamoto kwa michezo ya ugenini lakini wamejiandaa kuendeleza rekodi ya ushindi mfululizo
"Kuna changamoto kucheza viwanja vya ugenini, lakini mpira uko hivyo..., tunaendelea na maandalizi, naamini wachezaji bado wana morali ya juu na ingawa tutakosa baadhi ya wachezaji hiyo haitakuwa sababu ya kushindwa kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa Iringa," amesema Mwandila.
Katika mchezo huo Yanga itamkosa beki wake Abdallah Shaibu 'Ninja' ambaye amefungiwa mechi tatu
Tangu ilipopanda daraja, Lipuli haijapata ushindi dhidi ya Yanga ikifungwa michezo miwili na kupata sare mchezo mmoja