Zahera awajibu wanaohoji kwa nini Ajib haanzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Mar 2019
Zahera awajibu wanaohoji kwa nini Ajib haanzi

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewataka wanaohoji kwa nini nahodha wa kikosi cha timu hiyo Ibrahim Ajib haanzi katika michezo ya hivi karibuni kuwa watulie kwani yeye ndiye anayefahamu mahitaji ya kila mechi

Katika mahojiano na Radio UFM, Zahera amesema huwa anapanga kikosi chake kufuatana na mahitaji ya mpinzani anayekutana nae

"Kwa wanaofuatilia wanafahamu, sio Ajib tu ambaye huwa anapumzika, nimekuwa nikibadili wachezaji mara kwa mara kufuatana na mahitaji ya mchezo," alisema Zahera

"Mabadiliko haya ni ya kawaida, haimaanishi kwamba Ajib kashuka kiwango au nina ugomvi nae"

"Wapo watu ambao kazi yao ni kufanya uchonganishi Yanga, nawashauri wafanye mambo mengine yenye faida kwao"

Baada ya kuwa na mwenendo mzuri tangu akabidhiwe kitambaa cha unahodha, Ajib amehusika kwa kucheza michezo mingi ya Yanga kabla ya michezo mitatu iliyopita ambayo yote hakuanza

Ajib amefunga mabao sita msimu huu na kutoa pasi za mabao 15.

Mpaka sasa ndiye mchezaji mwenye mafanikio zaidi kwenye ligi kwani kati ya mabao 45 ayliyofungwa na Yanga, Ajib amehusika katika mabao 21

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’