Mavunde aahidi kukusanya mamilioni Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Mar 2019
Mavunde aahidi kukusanya mamilioni Yanga

Siku chache baada ya kuteuliwa kuongoza Kamati Maalumu ya Kuhamasisha Uchangishaji wa fedha Yanga, Anthony Mavunde ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo ameahidi kuhakikisha lengo la uongozi wa timu hiyo linafanikiwa ikiwemo kuondokana na changamoto ya kiuchumi inayoikumba.

Mavunde ambaye ni Mbunge wa Dodoma Mjini na Naibu Waziri wa Kazi Ajira na Watu Wenye Ulemavu, anaiongoza kamati hiyo ya watu 26 na ameliambia gazeti la Mwanaspoti kuwa amekubaliana na uteuzi huo na atahakikisha anafanya kila linalowezekana kufanikisha lengo la Yanga.

"Nimepokea kwa mikono miwili heshima hii, nitahakikisha lengo la kamati hii linafikiwa, nitapambana kwa kila hali nikishirikiana na wanakamati wenzangu ili kuisaidia timu," alisema.

Aliwaasa wanachama na wapenzi wa Yanga kote nchini kuungana nao na kushiriki kuchangia timu hiyo ili iendelee kufanya vizuri zaidi msimu huu ikiwemo kuchukua taji la Ligi Kuu na Kombe la FA.

Aidha Mavunde ambaye ni Mlezi wa Tawi la Yanga Makao Makuu, Dodoma aliwapongeza wanachama na wapenzi wa Mkoa wa Dodoma kwa kuwa mstari wa mbele kuichangia timu hiyo ambapo mwenyekiti wa tawi hilo, Dominic Albinus ‘Baba Paroko’ alikubali kuchangia Sh 1 milioni kila mwezi.

"Tawi letu chini ya mlezi wetu, Mavunde mbali na kuhamasisha wapenzi wa Yanga kuwa wanachama lakini pia kwa pamoja tumekubaliana kuchangia kila mwezi Sh 1 milioni kwa timu yetu ili iendelee kufanya vema zaidi msimu huu kwa kubeba mataji na kufanya usajili wa msimu ujao," alisisitiza.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’