Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ameondoka leo kurejea kwao DR Congo kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa, yeye akiwa ni kocha msaidizi
Zahera anamsaidia Florent Ibenge ambaye ndiye kocha Mkuu wa timu hiyo pia akiinoa klabu ya AS Vita
Kutokana na majukumu ya michuano ya ligi ya mabingwa yanayoikabili Vita Club ambayo inatarajiwa kutua nchini kesho tayari kuikabili Simba Jumamosi, Zahera amerejea mapema Congo kukiandaa kikosi cha timu ya Taifa ambacho March 24 kitachuana na Liberia katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019
DR Congo inahitaji kushinda mchezo huo unaopigwa nyumbani Stade Des Martyrs ili iweze kufuzu fainali za michuano hiyo zitakazopigwa mwezi Juni nchini Misri
March 24 pia Tanzania itashuka uwanja wa Taifa kuikabili Uganda Cranes katika mchezo ambao matokeo ya ushindi huenda yakaihakikishia Tanzania kufuzu baada ya kusubiri miaka 38