Mchezaji wa Alliance FC Juma Nyangi amefungiwa mechi tatu mfululizo na Kamati ya Nidhamu ya TFF baada ya kumfanyia kitendo cha udhalilishaji Gadiel Michael wakati timu hizo zilipokutana kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara March 2, 2019.
Kulingana na Maamuzi yaliyotolewa na Kamti ya Nidhamu ya TFF mapema leo, Nyangi alikiri kutenda kosa hilo na kuomba msamaha
Kamati baada ya kupitia utetezi pamoja na ushahidi imemtia hatiani Juma Nyangi kwa kosa hilo la udhalilishaji.
Mbali na kumfungiwa mechi tatu, Nyangi amepigwa faini ya shilingi milioni mbili (2,000,000) na adhabu zote zinakwenda pamoja.
ADVERTISE HERE