Baadhi ya mashabiki wa Simba wanamlaumu beki wa KMC Ally Ally kuwa jana aliizawadia Yanga bao katika mchezo ambao vinara hao wa ligi kuu waliibuka na ushindi wa mabao 2-1
Jana idadi kubwa ya mashabiki wa timu hiyo walijitokeza uwanja wa Taifa kuiunga mkono KMC wakiamini wangeweza kupoza machungu kama Yanga ingepoteza mchezo huo
Juzi Simba ilichapwa mabao 2-0 na JS Saoura, kipigo ambacho kimewaweka kwenye wakati mgumu mashabiki wa timu hiyo dhidi ya watani zao Yanga
Hata hivyo Ally Ally hakuwa na la kufanya zaidi ya kujifunga kutokana na aina krosi iliyopigwa na Ajib na jinsi mchezaji huyo alivyokuwa amejipanga katika kuokoa
Ally Ally alijaribu kuokoa mpira wa kichwa huku akiwa amelielekea lango lake, mara nyingi mipira ya aina hiyo huishia nyavuni
Lakini pia kama Ally Ally angeuacha mpira ule ni dhahiri ungemaliziwa kirahisi sana na Heritier Makambo ambaye alikuwa katika nafasi nzuri ya kufunga
Pongezi nyingi anastahili mpigaji wa krosi Ibrahim Ajib ambaye aliweza kupiga hesabu zake vyema na kumpa wakati mgumu Ally Ally