Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga leo Jumapili, March 10 2019 wanashuka katika uwanja wa Taifa kuikabili KMC kwenye mchezo wa raundi ya 30 wa ligi hiyo
Kikosi cha Yanga kiliingia kambini juzi hoteli ya Nefaland kujiandaa na mchezo huo ambao matokeo ya ushindi yatazidi kuikita Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi
Kuelekea mchezo huo, kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema anafahamu mchezo hautakuwa mwepesi kutokana na aina ya uchezaji wa KMC lakini amewaandaa vijana wake kuhakikisha wanapata matokeo mazuri
Mchezo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa kumi kamili jioni ambapo viingilio ni VIP A Tsh 15,000/-, VIP B na C Tsh 10,000/- na mzunguuko Tsh 5,000/-
Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 64, alama nane mbele ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 56