Zahera afunguka urejeo wa Manji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Mar 2019
Zahera afunguka urejeo wa Manji Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema alipata nafasi ya kufanya mazungumzo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji pamoja na viongozi wengine wa Yanga ambapo kuna uwezekano bilionea huyo atarejea Yanga

Aidha Zahera amesema anaamini Yanga bado inamuhitaji Manji kwani amebaini ni kiongozi mwenye maono na ufahamu mkubwa wa mambo

"Tumezungumza mambo mengi sana kuhusiana na Yanga na amezungumza na sisi kwa uwazi kabisa, ila nlichokiona anasubiri kwanza hali ikae sawa, " Zahera amenukuliwa na gazeti la Sport Xtra

"Inaonekana kuna sehemu ndani ya Yanga kuna baadhi ya vitu vinakwenda kwenye hali fulani ambayo haimpendezi sana ndiyo maana hajaweka fedha yake kwenye uendeshaji"

"Maana unajua yule ni mfanyabiashara hawezi kuweka fedha tu bila kuwa na mamlaka nazo"

"Unajua mimi nikikaa na wewe dakika tano naweza kujua una akili au huna. Ila baada ya kikao cha Manji niliwaambia wale viongozi kwamba huyu jamaa anajua, ana akili sana"

"Ukimsikiliza mipangilio yake na kile anachokisema ni ukweli kabisa na ni vitu ambavyo vinatekelezeka na vinaweza kuifanya Yanga ikapiga hatua"

"Kwa jinsi nilivyomsikiliza na kumuelewa Manji atarudi Yanga, atarudi tu ni suala la muda tu," amesema Zahera

Tangu Manji ajiuzulu kuiongoza Yanga, timu hiyo yenye historia ya kipekee Tanzania imeyumba sana kiuchumi

Kukosekana kwake kumechangia kwa kiasi kikubwa msimu uliopita Yanga kushindwa kupata nafasi ya kushiriki michuano ya CAF msimu huu

Awali Manji alikuwa tayari kurejea katika nafasi yake Januari 15 mwaka huu baada ya Wanachama kuikataa barua yake ya kujiuzulu

Hata hivyo Serikali iliiagiza Yanga kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zote zilizowazi ikiwemo nafasi ya Mwenyekiti, uchaguzi ambao nao ulishindwa kufanyika Januari 13 baada ya baadhi ya Wanachama kwenda Mahakamani kuupinga

Tayari TFF na Yanga zimefikia makubaliano ya kuanza upya mchakato huo wa uchaguzi ambapo wagombea watalazimika kujaza fomu upya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’