Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amesema hapendezwi na utaratibu wa kupangua ratiba ya ligi kuu mara kwa mara kwani unavuruga mipango ya timu.
Lwandamina aliyewasili jana kutokea kwao nchini Zambia alikokuwa amehudhuria msiba wa baba yake, amesema mipango ya klabu yake ilikuwa ni kusafiri leo kuelekea mkoani Njombe kuivaa Mji katika mchezo uliokuwa awali umepangwa kupigwa Septemba 06 lakini sasa umesogezwa mbele mpaka Jumamosi ya Septemba 09.
"Inasikitisha kuona ratiba ya ligi ikibadilika mara kwa mara,jambo hili lina athari kubwa," amesema Lwandamina.
"Tulipanga kusafiri leo kwa ajili ya mchezo wa tarehe 6,lakini sasa tunalazimika kuongeza siku zaidi,hii ina maana kuwa 'program' zote zilizowekwa awali zinavurugika"
TFF imesogeza mbele michezo yote iliyokuwa imepangwa kupigwa Septemba 06 na sasa itachezwa Septemba 09 na 10. Huku michezo iliyokuwa imepangwa kuchezwa katika siku hizo nayo ikisogezwa mbele.

ADVERTISE HERE