Michango yenu iko salama - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Mar 2019
Michango yenu iko salama - Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewahakikishia wapenzi, mashabiki na Wanachama wa klabu ya Yanga kuwa pesa wanazoichangia timu yao ziko salama na wapuuze taarifa zinazosambazwa zinazodai kuwa kuna fedha zimetolewa 'kinyemela'

Akizungumza mapema leo katika mazoezi ya Yanga yanayofanyika uwanja wa chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es salaam, Zahera amesema wanaotoa taarifa hizo wana lengo la kuwavunja moyo Wana Yanga ili wasiendelee kuichangia timu yao

"Nawaambia watu wengi wanapenda timu yetu iharibike. Kuna watu wanafanya matangazo mengi ya kusema kama mchango unaofanyika viongozi wanakula pesa"

"Wanasema kuna viongozi wanakula milioni tatu, ni uongo. Hakuna hata elfu moja, senti moja ambayo inatoka katika pesa hiyo ambayo watu wanachangia." amesema Zahera

"Hakuna hata kiongozi mmoja ambaye ana ruhusa ya kugusa iyo pesa"

Naye nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib amesema hakuna namna yoyote ambayo fedha hiyo inaweza kutolewa bila kuidhinishwa na watia saini watatu ambao ni yeye(Ajib), Kocha Mwinyi Zahera na Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh

"Kama fedha inatakiwa kutolewa ni lazima wote watatu tusaini, hivyo taarifa inayosambazwa ni uongo kwani jambo hilo haliwezekani"

Jana kupitia Redio One, mtu aliyejitambulisha kama mwanachama wa Yanga Suleiman Kato alidai kiasi cha pesa milioni tatu zilizochangwa na mashabiki wa Yanga kupitia mitandao ya simu zilitolewa kwenye mtandao husika na kuhamishiwa kwenye Bank moja iliyopo Kariakoo ambapo aliwatuhumu Kaimu katibu Omary Kaaya pamoja na Mhasibu na baadhi ya viongozi kushirikiana katika hujuma hiyo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’