Hatuwahofii Alliance Fc, tukutane Mwanza - Ten

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Mar 2019
Hatuwahofii Alliance Fc, tukutane Mwanza - Ten

Misimu miwili iliyopita Yanga ilitolewa kwenye michuano ya kombe la Azam (ASFC) na Mbao Fc katika hatua ya nusu fainali ambapo mchezo ulipigwa dimba la CCM Kirumba

Yanga itarudi tena Mwanza katika uwanja huohuo kuikabili Alliance Fc lakini ikiwa ni mchezo wa hatua ya robo fainali

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema hawana hofu ya kuikabili Alliance Fc kwa mara nyingine na watajiandaa kikamilifu ili waweze kushinda mchezo huo na kutinga hatua ya nusu fainali

Baada ya kukosa ushindi kwa misimu kadhaa kwenye dimba la CCM Kirumba, msimu huu Yanga imetakata katika dimba hilo kwa kufanikiwa kuzifunga Mbao Fc na Alliance

"Tunafahamu Mwanza ni pagumu, ili kupata ushindi kwenye uwanja wa CCM Kirumba unapaswa kuwa umejiandaa kwelikweli," amesema Ten

"Msimu huu tumefanya vizuri katika michezo yote miwili tuliocheza Mwanza, naamini tunao uwezo wa kupata matokeo kwa mara nyingine"

"Tunaiheshimu Alliance, tunafahamu ni timu nzuri lakini kucheza na Yanga ni kitu tofauti"

Kama Yanga itashinda mchezo huo utakaopigwa kati ya March 25-28, kwenye hatua ya nusu fainali itachuana na mshindi kati ya Lipuli Fc dhidi ya Singida United, mchezo ambao utakuwa wa ugenini

Mchezo wa fainali utapigwa uwanja wa Ilulu mkoani Lindi mwishoni mwa msimu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
2d ago
READ MORE β†’