Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema licha ya timu yake kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Alliance Fc juzi, wachezaji wake hawakucheza vizuri
Zahera amesema atatumia mazoezi ya wiki hii kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo huo kabla ya kuikabili KMC Jumapili ijayo kwenye uwanja wa Taifa
"Mechi ilipomalizika niliwapa pongezi wachezaji wangu, lakini nitawaelekeza mazoezini jinsi ilivyokuwa kwa sababu kuna vitu sikufurahishwa navyo kutokana na wachezaji wenyewe hawakuheshimu mtego tulioutayarisha," amesema Zahera

Kikosi cha Yanga tayari kimerejea jijini Dar es salaam ambapo kesho Jumanne kinatarajiwa kuendelea na maandalizi ya mchezo huo dhidi ya KMC utakaopigwa Jumapili, March 10
Yanga bado iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 64, alama 11 zaidi ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili ikiwa na alama 53
Simba iliyoshuka dimbani mara 20 inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 51
Simba bado ina idadi kubwa ya michezo ya viporo ambapo hali hiyo inailazimu Yanga kuhakikisha haifanyi tena makosa ili kuipa wakati mgumu timu hiyo kwenye michezo yake ya viporo ambayo mingi itachezwa wakati ligi itakapokuwa imesimama kupisha michuano ya AFCON U17 itakayopigwa mwezi ujao jijini Dar es salaam