Kwa kiwango anachoonyesha sasa mlinda lango wa Yanga Klaus Kindoki huwezi kuamini kama ni yule aliyekuwa akitunguliwa mabao mepesi
Pengine mashabiki walichangia kumtoa mchezoni wakati ule ambao alikuwa akizomewa na wale waliokuwa wamekosa imani nae
Kindoki wa sasa anajiamini, hana hofu tena awapo langoni. Anaonyesha uwezo wake halisi
Kindoki ameimarisha kiwango chake wakati ambao Yanga inahitaji kila mchezaji kuwa katika ubora wake ili kupigania ubingwa wa ligi kuu
ADVERTISE HERE