Yanga ijipange kweli michuano ya Mabingwa Afrika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Sep 2017
Yanga ijipange kweli michuano ya Mabingwa Afrika
Msimu huu viongozi wa Yanga wameweka bayana kuwa na shauku ya kuiona Yanga ikifanya vizuri kwenye michuano ya Afrika ambapo Yanga inashiriki klabu bingwa kwa msimu wa tatu mfululizo.

Lengo la msimu huu ni kuhakikisha Yanga inatinga hatua ya makundi ya michuano hiyo ambayo bingwa hupata karibu Bilioni 2.

Aidha kutinga hatua ya makundi tu timu inajihakikishia kuweka kibindoni si chini ya milioni 527.

Kwa utaratibu mpya, ni timu 16 zinazotinga hatua ya makundi tofauti na nane zilizokuwa zinatinga hatua hiyo miaka ya nyuma.

Utaratibu mpya umenza kutumika msimu uliopita ambapo kama Yanga ingefanikiwa kuifunga Zanaco basi ingetinga hatua ya makundi kwa mara ya pili baada ya mafanikio iliyopata kwenye michuano hiyo mwaka 1998.

Mwaka juzi Yanga ilitinga makundi michuano midogo ya CAF CC inayofahamika kama kombe la shirikisho ambayo Simba itashiriki msimu huu.

Aidha Yanga ikivuka mzunguuko wa kwanza na kutolewa katika mzunguuko wa pili basi itahamishiwa kwenye michuano ya kombe la shirikisho.

Kwa nini michuano hii ni kipaumbele

Kwanza zawadi nono za michuano hii ni sababu tosha za kuipa kipaumbele.

Ligi kuu ya Vodacom ambayo Yanga imetwaa kwa misimu mitatu mfululizo, bingwa anapata kombe na kitita cha Milioni 80.

Lakini kwa timu inayotinga hatua ya makundi peke yake katika michuano ya Klabu bingwa inapata karibu Mil 527 wakati ile inayoingia hatua ya makundi kombe la shirikisho inapata Mil 331.

Zawadi za ubingwa wa VPL kwa misimu mitatu mfululizo ni Mil 240 nina uhakika ni chache kuliko kitita ilichopata Yanga iliposhiriki hatua ya makundi kombe la shirikisho msimu wa 2015/16.

Pili hii ni nafasi nyingine ya kuiweka juu Tanzania kwenye ramani ya soka la Kimataifa.

Miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia mabadiliko makubwa kwenye soka la Kimataifa ngazi ya vilabu na hata timu za Taifa.

Naamini hata vilabu vya Tanzania vinaweza kufanya 'maajabu' kama yanayofanywa na wengine.

Ni jambo la kutia moyo kuona timu zote za Tanzania, Yanga na Simba zimefanya usajili makini kwa kuzingatia ushiriki wa michuano hiyo.

Michuano hiyo pia itatoa fursa kwa wachezaji kuonekana kimataifa na kuwapa nafasi ya kwenda kusakata kabumbu nje ya nchi.

Ni utaratibu huo utakaonufaisha Taifa kwani ni dhahiri timu ya Taifa itaboreka zaidi.

Hata hivyo haitakuwa kazi rahisi kutinga hatua ya makundi. Timu ni lazima iandaliwe Kimataifa.

Miongoni mwa timu ambazo Yanga itakutana nazo kwenye mzunguuko wa pili ni Al Ahly na Misr Lel Makkasa za Misri, Esperance na Etoile Du Sahel za Tunisia, TP Mazembe na AS Vita za DR Congo, ES Setif na MC Alger iliyoitoa Yanga kwa jumla ya mabao 4-1 kwenye play-off za Kombe la Shirikisho Afrika.

Pi Mamelodi Sundowns na Bidvest Wits za Afrika Kusini, ASEC Memosas na Mbabane Swallows aliyoichezea kiungo wake mpya, Kabamba Tshishimbi.

Yanga pia inaweza kukutana na Msuva akiwa na El Jadida yake waliokata tiketi sambamba na Wydad Casablanca.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’