Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa wachezaji watano hawatakuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachoikabili Alliance Fc kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba
Taarifa ya Yanga imesema beki Andrew Vicent anasumbuliwa na maumivu ya misuli, hakujumuishwa katika kikosi kilichosafiri Mwanza
Raphael Daudi, Baruani Yahya na Juma Mahadhi hawa bado ni majeruhi wanaoendelea na matibabu wakati kiungo Pius Buswita yeye hakusafiri
Habari njema kwa Yanga ni kurejea kikosini kwa kiungo Thabani Scara Kamusoko ambaye amepona majeraha na huenda kesho akajumuishwa katika kikosi kitakachoivaa Alliance Fc
ADVERTISE HERE