Kikosi cha Yanga leo kimefanya mazoezi ya mwisho katika dimba la CCM Kirumba tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Alliance Fc hapo kesho

Leo ilikuwa siku ya pili kwa Yanga kujifua jijini Mwanza ambapo kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo
"Wachezaji wako vizuri. Tmefanya mazoezi mara mbili Dar es salaam na hapa Mwanza tumefanya mazoezi mara mbili pia, nadhani tutakuwa vizuri sana kwenye mchezo wa kesho, " amesema Zahera
"Tunajua tunacheza na timu ambayo kuanzia mzunguuko wa pili imefanya vizuri, hata hivyo tumeshacheza na timu nyingine ambazo ziko vizuri na tukaweza kupata matokeo pia"
"Hivyo naamini vijana wangu kesho wataweza kutupatia alama tatu muhimu"
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa kumi kamili jioni