Lwandamina apendekeza mtaalam wa matibabu ya viungo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Sep 2017
Lwandamina apendekeza mtaalam wa matibabu ya viungo
Kocha wa Yanga, George Lwandamina amerejea jana kutoka kwenye msiba wa baba yake.

Habari mpya ni kwamba ameiambia klabu hiyo iongeze mtaalamu mwingine kwenye benchi la ufundi kulingana na Mwanaspoti

Alichogundua Lwandamina katika kikosi chake ni kwamba washambuliaji wake watatu; Obrey Chirwa, Amissi Tambwe na Geofrey Mwashiuya, walikuwa na majeruhi kwa muda mrefu wakiuguza tatizo la aina moja, maumivu ya magoti.

Habari za uhakika ambazo Lwandamina mwenyewe kathibitisha ni kwamba kocha huyo ameomba kutafutiwa mtaalamu wa matibabu ya viungo atakayesaidiana na daktari wa timu hiyo Dk. Edward Bavu.

Mmoja wa viongozi wa Yanga alisema tayari maombi hayo ambayo hata wao wameyakubali, yameshaanza kufanyiwa kazi kwa kumtafuta mtaalamu huyo kwa kuangalia ndani na nje ya nchi atakayefanya kazi hiyo.

Lwandamina alisema: Ò€œNikweli nimewaomba wanitafutie huyo mtu, sawa sasa tuna daktari wa timu lakini tunatakiwa sasa kufikiria mbali zaidi kumaliza hali kama hii ya kuwa na wachezaji wengi muhimu majeruhi kama hivi na hili linaweza kuwa tatizo zaidi unapokuwa katika mashindano makubwa ya Afrika ambayo hayana muda wa kupoteza kila mchezo ni muhimu.Ò€

Wakati huo huo upo uwezekano winga wa zamani wa Yanga na timu ya Taifa, Said Maulid 'SMG' akaongezwa kwenye benchi la ufundi la Yanga kwa ajili ya kazi maalumu.

SMG ni mtaalamu wa kukusanya takwimu mbalimbali za wachezaji.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
2m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
27m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
35m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’