Rasmi, uwanja wa Taifa kufungwa wakati wowote

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Feb 2019
Rasmi, uwanja wa Taifa kufungwa wakati wowote

Timu zinazotumia Uwanja wa Uhuru, Taifa na Azam Complex kwaajili ya michezo ya ligi mbalimbali zimeshauriwa kutafuta viwanja vingine kwa ajili ya michezo yao kutokana na viwanja hivyo kukaribia kufungwa kupisha ukarabati kuelekea kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Vijana.

Wito huo umetolewa jana na Meneja wa Uwanja wa Taifa Nsajigwa Gordon ambaye amesema hatua hiyo inatokana na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuagiza viwanja hivyo kufungwa ili kupisha marekebisho.

Yanga ni miongoni mwa timu zinazotumia uwanja wa Taifa kama uwanja wake wa nyumbani. Hivyo italazimika kutafuta uwanja mwingine kwa ajili ya michezo yake ya nyumbani

Hapa ndipo umuhimu wa timu kumiliki uwanja wake unapoonekana

Kufuatia hatua hiyo,wengi wamependekeza uwanja wa CCM Kirumba ambao Yanga imewahi kuutumia mara kadhaa kwa michezo yake mbalimbali ya Kimataifa

Yanga pia ina uungwaji mkono mkubwa mkoani Mwanza.

Lakini pia hata dimba la Amaan visiwani Zanzibar linaweza kufaa kutumiwa na mabingwa hao wa Kihistoria

Viwanja vya Uhuru, Taifa na Azam Complex vinatarajiwa kufungwa ili kupisha ukarabati tayari kwa michuano ya AFCON 19 ngazi ya vijana chini ya umri wa miaka 17 inayotarajiwa kuanza April 14-28 Tanzania ikiwa mwenyeji wa michuano hiyo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’