Yanga yaanza mkakati wa kuwabakisha nyota wake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Feb 2019
Yanga yaanza mkakati wa kuwabakisha nyota wake

Ifikapo mwishoni mwa msimu idadi kubwa ya wachezaji wa Yanga watakuwa wamemaliza mikataba ya kuitumikia timu hiyo huku presha ya kuwapoteza baadhi ya nyota walion'gara ikipanda

Wakati ikisubiriwa ripoti ya mahitaji ya usajili itakayotolewa na kocha Mwinyi Zahera mwezi May msimu utakapomalizika, Yanga imelazimika kuanza mapema mkakati wa kuwabakisha baadhi ya wachezaji ambao tayari wameanza kumezewa 'mate' na timu pinzani

Miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao iko ukingoni na kuwepo ulazima wa kuhakikisha hawanyakuliwi na timu pinzani ni pamoja na Ibrahim Ajib na Papi Kabamba Tshishimbi

Wakati Ajib akin'gara zaidi katika kikosi cha Yanga kwa kufunga na kutoa pasi nyingi za mabao, Tshishimbi amerudi katika kiwango chake na hivyo kuwa miongoni mwa wachezaji wanaowaniwa zaidi na timu nyingine

Yanga ina idadi kubwa ya wachezaji ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na Amissi Tambwe, Raphael Daudi, Juma Mahadhi, Abdallah Shaibu, Pato Ngonyani, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Pius Buswita, Said Juma, Thabani Kamusoko, Mrisho Ngasa, Matheo Anthony na Gadiel Michael

Mwishoni mwa msimu Yanga huenda ikafanya mchakato mkubwa wa usajili kwa ajili ya msimu ujao hasa kama itapata nafasi ya kutinga michuano ya CAF kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu au kombe la FA

Hata hivyo hatma ya usajili huo itategemea na kiasi cha fedha zitakazokusanywa kutoka kwa michango ya mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kupitia mpango ulioasisiwa na kocha Mwinyi Zahera

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’