Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam kesho Alhamisi asubuhi kuelekea Mwanza kwa usafiri wa ndege tayari kwa mchezo wa ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Alliance
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, March 02 katika uwanja wa CCM Kirumba
Mratibu wa Yanga Hafidh Saleh amesema msafara wa timu hiyo utakuwa na wachezaji 20 pamoja na viongozi nane wakiwemo wa benchi la Ufundi
Tangu irudi kutoka Lindi, Yanga imekuwa ikijifua kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini kujiandaa na mchezo huo
ADVERTISE HERE