Mwishoni mwa wiki Yanga itarejea tena jijini Mwanza kuikabili Alliance Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa Jumapili, March 03 katika uwanja wa CCM Kirumba
Alliance Fc inayonolewa na kocha Malale Hamsini imeonekana kupania mchezo huo ambapo kocha huyo wa zamani wa Ndanda Fc ameongeza dozi ya mazoezi kwa vijana wake
Alliance Fc imeimarisha kiwango chake siku za karibuni hivyo kuufanya mchezo huo kutarajiwa kuwa na ushindani mkali
Katika mchezo wa mzunguuko wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa, Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0
Kikosi cha Yanga kilirejea jana kutoka Lindi na kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo
Kocha Mwinyi Zahera amesema wanafanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha wanashinda mchezo huo ili kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi