Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namungo Fc na kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya kombe la FA, kikosi cha Yanga kinarejea leo jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo unaofuata wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, March 02 kwenye dimba la CCM Kirumba
Yanga iliyotoka Mwanza wiki iliyopita kucheza na Mbao Fc, inalazimika kurejea tena jijini humo
Baada ya mchezo dhidi ya Alliance, Yanga itarejea jijini Dar es salaam kuikabili KMC katika mchezo utakaopigwa March 10
ADVERTISE HERE