Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina, anadaiwa kuzuia usajili wa kiungo mshambuliaji Mrisho Ngasa hadi atakaporejea na kuona kiwango chake kwenye maandalizi ya msimu ujao.
Lwandamina amaye yuko mapumziko nchini Zambia ameuambia mtandao wa GOAL kuwa anataka kujenga kikosi imara hivyo hawezi kukubali kusajili mchezaji ambaye hatokuwa na vigezo visivyokuwa na mchango kwenye timu hiyo kwani hataki kuwa na watu tegemezi.
“Nimeutaka uongozi uwe na subra kwanza nitakaporudi tukianza maandalizi ya msimu ujao mchezaji huyo anaweza kuungana na sisi hapo ndiyo nitaona kiwango chake lakini siyo kusajili kwasababu zamani alikuwa anacheza kwetu,â€amesema Lwandamina.
Mzambia huyo amesema lazima watu watambue kuwa Yanga inashiriki michuano mikubwa msimu ujao ya Ligi ya Mabingwa hivyo ili kuweza kufanya vizuri lazima iwe na wachezaji wenye viwango vya kupambana na kuipa timu matokeo yale yanayokubalika na siyo kufungwa.
Amesema yeye kama kocha hapendi kuona kila wakati timu hiyo ikishindwa kufanya vizuri kwwasababu ya aina ya wachezaji bali anataka wapambane na kupata matokeo na endapo inatokea wanafungwa basi iwe ni kuzidiwa kwa kawadia lakini siyo kuwa na wachezaji mizigo.
“Mimi simjui Ngasa lakini siwezi kukataa mchezaji mzuri ndiyo maana nimewaambia viongozi wasubiri kwanza nitakaporudi ili niweze kumuona mazoezini mchezaji huyo akitokea kunivutia tutamsajili,†amesema.
Kocha huyo amesema amejipa jukumu la kusimamia zoezi lote la usajili wao wa msimu ujao lengo ni kutambua uwezo wa kila mchezaji atakayesajiliwa na timu hiyo, ili kuepusha swala la kutegemea baadhi ya wachezaji wachache kama ilivyokuwa msimu uliopita.

ADVERTISE HERE