Ajib aitumia salamu Namungo Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Feb 2019
Ajib aitumia salamu Namungo Fc

Kikosi cha Yanga kimeondoka leo jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Lindi kwa ajili ya mchezo wa kombe la FA (ASFC) dhidi ya Namungo Fc, inayoshiriki ligi daraja la kwanza

Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumapili, Februari 24 2019, saa kumi kamili jioni katika uwanja wa Majaliwa

Nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib amesema wanaenda mkoani Lindi wakiwa na lengo la kusaka ushindi ili kuweza kutinga hatua inayofuata

Aidha, Ajib amesema ushindi waliopata dhidi ya Mbao Fc juzi, umewaongezea wachezaji ari na watapambana kuhakikisha wanashinda mchezo huo wa ugenini

"Ushindi tuliopata juzi kwenye mchezo dhidi ya Mbao Fc umetuongezea ari na sasa tunaelekeza nguvu zetu Lindi kuikabili Namungo. Lengo letu ni kufanya vizuri kwenye mchezo huo ili tuweze kutinga raundi inayofuata," amesema Ajib

"Tutaenda kupambana na kuhamasishana ili kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye kwenye mchezo huo"

Juzi Yanga iliichapa Mbao Fc mabao 2-1 katika mchezo ambao Yanga ilionyesha kandanda safi ya kushambulia kwa nguvu katika kipindi cha pili

Matokeo hayo yameongeza 'chachu' ya kusaka ushindi mchezo dhidi ya Namungo keshokutwa

Hii itakuwa mara ya pili kwa Yanga kuikabili Namungo Fc katika uwanja wa Majaliwa

Mwisho mwa mwaka 2018 timu hizo zilikutana kwenye mchezo wa kirafiki uliomalizika kwa sare ya bao 1-1

Hata hivyo kwenye mchezo huo Yanga iliwakosa baadhi ya wachezaji waliokuwa na timu ya Taifa sambamba na kocha Mwinyi Zahera aliyekuwa na timu ya Taifa ya DR Congo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’