Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema ushindi wa mabao 2-1 iliyopata Yanga dhidi ya Mbao Fc ulitokana na wachezaji wake kuwa na nia ya kushinda mchezo huo
Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya mchezo, Zahera alisema waliweka nia ya kushinda mchezo huo ili kumaliza 'uteja' kwa Mbao Fc kila wanapocheza dimba la CCM Kirumba
"Wakati tunaondoka Hotelini kuelekea uwanjani, niliwaambia wachezaji wangu, yule ambaye anaamini leo tutapata ushindi na apande kwenye basi, asiyeamini abaki Hotelini," alisema Zahera
"Niliwaambia kila kitu kina mwisho, mambo ya kufungwa fungwa na Mbao leo iwe mwisho"
Licha ya kutangulia kufunga bao la kuongoza, Mbao Fc ilishindwa kuhimili kasi ya Yanga kwenye kipindi cha pili
Heritier Makambo na Amissi Tambwe waliihakikishia Yanga ushindi wa kihistoria dhidi ya Mbao Fc baada ya kushindwa kupata matokeo kwa misimu miwili mfululizo katika uwanja wa CCM Kirumba