Ushindi wa leo dhidi ya Mbao Fc umedhihirisha utayari wa Yanga kupambana mpaka dakika ya mwisho katika mbio za ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu
Wapo wengi hawakuipa Yanga nafasi ya kushinda leo wakiangalia zaidi historia kuwa Yanga haijawahi kuifunga Mbao kwenye dimba la CCM Kirumba
Lakini pia, upambanaji wa wachezaji hasa katika kipindi cha pili umeonyesha uimara wa kikosi cha Zahera na hakika kama hakutakuwa matukio ya 'mbeleko' Yanga inao uwezo wa kutwaa ubingwa msimu huu
Ushindi wa mabao 2-1 uliopatikana ni matokeo ya ujasiri na kujituma kwa wachezaji wa Yanga ambao wameonyesha kuwa tayari kuipigania timu hadi tone la mwisho
Leo tumeshuhudia kila mchezaji akijitoa kuhakikisha Yanga inapata matokeo katika uwanja ambao umekuwa mgumu kwao kuondoka na alama tatu misimu miwili iliyopita