Winga Mrisho Ngasa leo atakiongoza kikosi cha Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mbao Fc, mchezo utakaopigwa dimba la CCM Kirumba
Ngasa mzaliwa wa Mwanza, amesema wamepania kuifuta rekodi ya Mbao Fc ya ushindi mfululizo dhidi ya Yanga kwa michezo iliyopigwa CCM Kirumba
"Hautokuwa mchezo mwepesi, lakini Mbao wasitarajie sisi kupoteza mchezo uliopita kutawapa wao nafasi ya kupata ushindi, tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi tatu," amesema Ngassa.
"Matokeo ya mchezo uliopita yamepita na tumeyaweka pembeni, kwa sasa tumeelekeza nguvu zetu kwenye michezo ya mbele, tunaanza na Mbao Fc leo"
Katika mchezo wa leo, Ngasa atakuwa akicheza kwenye uwanja wa nyumbani
ADVERTISE HERE