Yanga imemalizana na wakala wa Zulu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
3 Sep 2017
Yanga imemalizana na wakala wa Zulu
Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na uongozi wa Yanga limemaliza mgogoro wa kimasilahi kati ya wakala wa aliyekuwa kiungo wa Yanga, Justin Zullu ‘Mkata Umeme’, Karin Nir baada ya uongozi wa Yanga kuvunja mkataba wa kiungo huyo.

Wakala huyo alipeleka mkataba wa mteja wake katika ofisi za TFF akitaka kuizuia Yanga kumtumia kiungo Papi Kabamba Tshishimbi akidai utaratibu haukufuatwa kuvunjwa kwa mkataba wa Zulu.

Novemba, mwaka jana, Yanga ilimsainisha Zullu mkataba wa mwaka mmoja mbele ya wakala huyo raia wa Israel, lakini hivi karibuni Yanga iliachana naye kutokana na kiwango chake kutowaridhisha.

Nir amesema kuwa, TFF imetumia busara kulimaliza suala la mteja wake na Yanga kwani tayari alipanga kwenda kushitaki Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

“Nimeshaondoka Tanzania lakini jambo kubwa ni kwamba Yanga wamekubali kuvunja mkataba wa mchezaji wangu, mkataba umevunjwa kwa makubaliano ya pande zote mbili tena kwa usawa," amesema.

"Namshukuru Katibu Mkuu wa TFF kutokana na kuweza kulimaliza suala hili kwa amani, niwashukuru Yanga kwa kuonyesha ushirikiano hasa katibu wao, Boniface Mkwasa.

"Hatuwezi kuendelea na malumbano tena kati yetu kwani tutaendelea kushirikiana kama ilivyokuwa awali,” amesema Nir.

Justin Zullu alipanga kuishitaki Yanga Fifa ili alipwe dola 100,000 (Sh milioni 221) baada ya mkataba wake kuvunjwa kiholela
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →