Yanga yamuwekea ngumu Mwanasheria wa Kakolanya, aenda TFF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
19 Feb 2019
Yanga yamuwekea ngumu Mwanasheria wa Kakolanya, aenda TFF

Sakata la mlinda lango Beno Kakolanya limepelekwa kwa shirikisho la soka Tanzania (TFF) baada ya Mwanasheria wa mlinda lango huyo Leopnard Richard kushindwa kufikia mwafaka na uongozi wa Yanga

Mwanasheria huyo aliuandikia barua uongozi wa Yanga akitaka kuvunjwa kwa mkataba wa mteja wake ambaye hayuko katika kikosi cha Yanga tangu Novemba 2018

Kakolanya aligoma kuitumikia Yanga akishinikiza alipwe sehemu ya fedha za usajili ambazo hakuwa amemaliziwa na malimbikizo ya mishahara

Hivi karibuni uongozi wa Yanga kupitia kwa Kaimu Mwenyekiti wake Samwel Lukumay ulitoa taarifa kuwa mlinda lango huyo haidai Yanga kwani tayari alishalipwa stahiki zake zote

Hata hivyo walishangazwa na hatua ya Kakolanya kupitia Mwanasheria wake kuandika barua ya kutaka kuvunjwa kwa mkataba wake

Kakolanya alisaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga mwanzoni mwa msimu. Hivyo licha ya kuwa hayuko kikosini, nyota huyo bado ni mali ya Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
11h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
15h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
20h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’