Timu ya Taifa ya Tanzania imeizamisha Botswana kwa mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Uhuru, mchezo wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA.
Mabao yote ya Stars yalifungwa na mshambuliaji anayechezea Difaa Al Jadida ya Morocco, Simon Msuva katika kila kipindi cha mchezo.
Bao la kwanza alilipachika kwenye dakika ya tano tu baada ya kupasiana na Mzamiru Yassini.
Baada ya kupachika bao hilo Stars ilionekana kupooza na kuipa Botwsana nafasi ya kutawala mchezo. Hata hivyo washambuliaji wa timu hiyo walikosa utulivu langoni kwa Stars.
Aidha mlinda lango namba moja wa Stars, Aishi Manula alikuwa kikwazo kikubwa kwa kuzuia michomo mikali ya Wa Botswana hao.
Kwenye kipindi cha pili Stars iliuanza mchezo huo kama ilivyokuwa katika kipindi cha kwanza na kufanikiwa kuandika bao la pili kwenye dakika ya 62, Msuva akifunga baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Shiza Kichuya.

Katika mchezo huo nahodha wa Stars Mbwana Samatta alishindwa kuonyesha makali yake kutokana na kukabwa muda wote na walinzi wa Botswana.
Hata hivyo walijikuta wakiadhibiwa na Msuva ambaye anaonekana kuimarika sana kwani ameongeza umakini anapokuwa langoni.

Mwezi Marchi Stars ilicheza mchezo wa kirafiki na Botswana na kupata ushindi kama huo wa mabao 2-0 wakati huo mabao yote yakifungwa na Mbwana Samatta.
Kwa mara ya kwanza kiungo wa Mumias Sugar ya Kenya, Abdallah Khamisi ameichezea timu ya Taifa sambamba na Emanuel Martini aliyeingia kuchukua nafasi ya Msuva dakika 10 za mwisho.
Ushindi huu dhidi ya Botswana utaimarisha nafasi ya Tanzania kwenye viwango vya FIFA kwa kuwa uko ndani ya kalenda ya shirikisho hilo.

ADVERTISE HERE