Kiungo wa Yanga Feisal Salum 'Fei Toto' amesema kupoteza mchezo wa leo ni matokeo tu, wataendelea kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri michezo inayofuata
Akizungumza baada kukamilika kwa dakika 90 zilizoipa Simba ushindi wa bao 1-0, Fei Toto amesema Simba walitumia nafasi waliyoipata ndio maana wameibuka na ushindi
"Tulijipanga vizuri, tumepoteza mchezo kama sehemu ya matokeo tu. Kama mchezaji au mshabiki lazima ukubali kuwa mpira una matokeo matatu, kufungwa, kushinda na droo. Mungu kawajalia Simba wamepata ushindi, tunawapongeza" amesema
"Hatukati tamaa, tutaendelea kupambana. Mungu kawajalia wao matokeo leo"
Kikosi cha Yanga kitaelekea mkoani Mwanza kuikabili Mbai Fc katika mchezo mwingine wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa February 20 2019