Saa chache zijazo vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga watakuwa dimba la Taifa wakipepetana na watani zao Simba, katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Mchezo huu ni wa Yanga kwani ndio iko nyumbani. Tayari mashabiki wake wameanza kuelekea uwanja wa Taifa kwa wingi
Mageti ya uwanja yalifunguliwa tangu saa nne hivyo kwa wale ambao bado hawajatoka, yawapasa wawahi mida hii
Kikosi cha Yanga kiko tayari kwa mchezo huo ambapo vijana wameandaliwa sawa sawa kuhakikisha leo wanawapa furaha Wana Jangwani
ADVERTISE HERE