Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kikosi chake kiko kamili tayari kwa mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa uwanja wa Taifa leo
Zahera amesema wachezaji wake wote 30 wako timamu kwa ajili ya mchezo huo ambao anaamini watapeleka furaha Jangwani baada ya kukamilika dakika 90
Yanga inayoongoza ligi kwa tofauti ya alama tisa dhidi ya Azam Fc na alama 22 dhidi ya wapinzani wao Simba, inaweza kujiwekea mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa kama itashinda mchezo wa leo
Kikosi cha Yanga kiliweka kambi mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo huo ambapo walirejea jijini Dar es salaam juzi usiku na jana wakafanya mazoezi ya mwisho
"Nawaita mashabiki wa Yanga waje uwanjani kwa wingi, tumejiandaa vizuri na wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo"
"Itakuwa ni mechi moja ya nguvu, njooni mtafurahi," Zahera aliwaambia waandishi wa habari jana