Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amefichua kuwa timu yake inakabiliwa na ushindani wa ndani na nje ya uwanja kutoka kwa wapinzani wao Simba
Zahera amesema anazo taarifa juu ya mabosi wa timu hiyo kuahidi kutoka kati ya Mil 10 na Mil 5 kwa timu ambazo zitashinda mchezo dhidi ya Yanga au kutoa sare
"Tulipokwenda Singida kucheza na Singida United, wale wachezaji wa Singida ambao waliwahi kucheza Yanga walituambia waliahidiwa Mil 10 kama wangeshinda lakini wakapata Mil 5"
"Hata tulipokwenda Tanga kucheza na JKT Tanzania wale watu wa timu hiyo ambao wanamapenzi nasi walikuja kutuambia wameahidiwa Mil 10 kama watatufunga"
"Sasa mimi nashangaa mtu umetumia pesa mingi kununua wachezaji, unawalipa mishahara mpaka dola 5,000 kila mwezi lakini bado unatoa tena pesa kwa timu pinzani ili kuizuia Yanga isishinde"
"Hakuna sababu ya kuwalipa mshahara wachezaji kama hawafanyi kazi yao. Maana haiwezekani uwalipe halafu bado utumie pesa kwa timu nyingine zikusaidie kushinda ubingwa"
"Hiyo inaonyesha sisi tumefanikiwa malengo yetu kwani mpaka wanafanya matukio hayo ina maana wanatuogopa. Wanajua hawawezi kufanikiwa bila kutumia nguvu ya ziada"
Kuelekea mchezo wa kesho Zahera amewataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa akiahidi kuwa Yanga itakayocheza kesho sio sawa na ile ya mzunguuko wa kwanza
"Wakati ule tumecheza nao tulitoka kucheza michezo minne, tulikuwa bado hatujakaa sawa. Mje kwa wingi uwanjani kesho mje mshuhudie Yanga nyingine kabisa"