Tukutane uwanja wa Mkapa kesho - Ten

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Feb 2019
Tukutane uwanja wa Mkapa kesho - Ten

Msemaji wa klabu ya Yanga Dismas Ten amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa kuiunga mkono timu yao itakapokuwa ikipepetana na watani zao Simba

Akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya klabu hiyo, Ten amesema wanahitaji nguvu ya mashabiki kesho ili kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu

Ten amesema muda wa mchezo wa kesho ni saa kumi kamili jioni na viingilio VIP A ni Tsh 30,000/-, VIP B na C ni Tsh 20,000/- na Mzunguuko Tsh 7,000/-

Katika hatua nyingine Ten amewataka Azam TV kuitendea haki timu hiyo kwani wamekuwa wakichagua matukio ya kurudia kwenye michezo ambayo Yanga iko dimbani

"Tulipocheza na Coastal Union kuna tukio mlinda lango wa Coastal Union alidakia mpira ndani ya nyavu lakini tukio hilo halikurudiwa kabisa," amesema

"Makambo alifunga bao safi katika mchezo dhidi ya Coastal lakini tukio hilo halikupewa uzito ukilinganisha na tukio la Ninja"

"Aidha katika mchezo dhidi ya JKT Tanzania Yondani alifanyiwa tukio baya sana lakini halikuonyeshwa"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’