Lwandamina kupangua safu ya ushambuliaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Sep 2017
Lwandamina kupangua safu ya ushambuliaji Yanga
Baada ya Obrey Chirwa kuepuka kifungo cha TFF na pia kupona majeraha yake, ni dhahiri atamlazimu kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina kupangua safu yake ya ushambuliaji.

Lwandamina amekuwa akiwatumia Ibrahim Ajib na Donald Ngoma kama washambuliaji wa kati. Hata hivyo wawili hao wameshindwa kuipa Yanga matokeo katika mchezo wa kwanza dhidi ya Lipuli.

Tabia za uchezaji wa Ngoma na Ajib zinafanana, wanapenda kucheza mpira muda wote hivyo kuwafanya wasitulie kwenye namba zao.

Ni tofauti na wachezaji Obrey Chirwa na Amissi Tambwe ambao hupenda zaidi kubaki kwenye namba zao wakivizia nafasi za kufunga.

Wawili hao msimu uliopita walifunga jumla ya mabao 23, Chirwa akifunga mabao 12 huku Amissi Tambwe akifunga 11.

Ngoma anaweza kuinufaisha zaidi Yanga kama atacheza na mmoja wa washambuliaji hao.

Chirwa ana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, nguvu na kasi. Pia mshambuliaji huyu mwenye umri wa miaka 23 huweza kuisaidia timu katika ukabaji pale inapoelemewa.

Upo uwezekano mkubwa Lwandamina akamtumia kama mshambuliaji wa kati huku Ngoma akamchezesha nyuma yake kama namba 10 wakati Ajib akimuhamishia pembeni.

Watatu hao wana nafasi ya kucheza pamoja wakati huu ambao Tambwe bado anasumbuliwa na majeraha lakini atakapokuwa fiti ni dhahiri haitakuwa jambo la kushangaza kumuona Ngoma au Ajib mmoja wao akianzia benchi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’