Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amethibitisha kuwa beki Abdallah Shaibu 'Ninja' atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoikabili Simba kesho kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Jana ilienezwa taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Kamati ya Nidhamu ya TFF imemfungia Ninja michezo mitatu kufuatia tukio la kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union wakati Yanga ilipocheza mkoani Tanga mapema mwezi huu
Ten amesema Yanga haijapokea barua yoyote kutoka kwa TFF kuhusiana na adhabu hiyo.
Suala la Ninja lilipelekwa Kamati ya Nidhamu ambayo hata hivyo iliahirisha kusikiliza shauri lake kwa kuwa beki huyo hakuwa jijini Dar es salaam
Ninja aliitwa kwenye kikao cha Kamati hiyo Februari 10, siku ambayo Yanga ilikuwa jijini Tanga ikichuana na JKT Tanzania
Hivyo Ninja ameruhusiwa aendelee kuitumikia Yanga hadi hapo Kamati ya Nidhamu itakapokutana na kutoa uamuzi
TFF imeachana na utaratibu wa kuwasimamisha wachezaji wakati wakisubiri mashauri yao yanapopelekwa Kamati ya Nidhamu
Kwani Kamati inapomkosa mchezaji na hatia, anakuwa tayari ameadhibiwa kwa kosa ambalo hakulitenda