Yanga ya sasa sio ile ya mwaka jana

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
13 Feb 2019
Yanga ya sasa sio ile ya mwaka jana

Katika mchezo wa duru ya kwanza uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana, kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alifanikiwa kimbinu na kuwaacha na mshangao wale waliokuwa wakiamini Yanga ingepoteza mchezo huo

Mchezo huo uliochezwa mwanzoni mwa msimu ulikuwa na presha kubwa kwa Yanga ambayo wakati huo ilikuwa bado haijakaa sawa.

Zahera alitambua kikosi chake kilikuwa bado hakijakaa sawa licha ya kuwa kilikuwa kimetoka kushinda michezo minne ya ligi dhidi ya Mtibwa Sugar, Stand United, Coastal Union na Singida United

Baada ya kuwa imecheza michezo 23 na kufanikiwa kushinda michezo 18, sare 4 na kupoteza mchezo mmoja, kwa sasa kikosi cha Yanga kiko tofauti kabisa na kile kilichocheza na Simba kwenye mchezo wa duru ya kwanza

Kwa wale ambao bado wanafikiria mazingira ya mchezo wa Jumamosi yatakuwa sawa na yale ya mchezo uliopita basi wajiandae kisaikolojia

1. Wachezaji wa Yanga wameongeza kujiamini

Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 58, alama 22 zaidi ya Simba inayoshika nafasi ya nne ikiwa na alama 36. Achana na hesabu ya idadi ya viporo kwani bado Simba italazimika kushinda ili alama zihesabiwe

Mwanzoni mwa msimu kutokana na changamoto zilizokuwa zikiikabili Yanga, timu hiyo ilikuwa ikicheza bila ya kuwa na malengo yoyote, hili aliwahi kulizungumza hata kocha Zahera

Lakini sasa baada ya mafanikio waliyoyapata kwenye ligi, timu hiyo imeweka malengo, inataka ubingwa wa ligi na kombe la FA

Hivyo kwa wachezaji wa Yanga huu ni mchezo wa kufa na kupona. Kwani wanajua kama watashinda, watajisafishia njia ya kueleka ubingwa

2. Viwango vya wachezaji Yanga vimeimarika

Katika mchezo wa Jumamosi Simba wasitarajie mteremko kwani baadhi ya wachezaji viwango vyao vimeimarika mara dufu kuliko wakati timu hizo zilipokutana mwaka jana

Miongoni mwa wachezaji hao ni nahodha Ibrahim Ajib. Hakun'gara kwenye mchezo uliopita lakini wasilitarajie hilo katika mchezo wa Jumamosi

Ajib wa sasa amepevuka na baada ya kuongezewa majukumu ya unahodha, amekuwa nguzo muhimu ya mafanikio ya Yanga

Mabao yake sita na 'assist' zake 13 zinamfanya kuwa silaha muhimu sana ya Yanga kuelekea mchezo huo

Pia Mrisho Ngasa, Feisal Salum, Paulo Godfrey, Abdallah Shaibu hawa ni miongoni mwa wachezaji ambao viwango vyao vimeimarika sana ukilinganisha na walivyokuwa mwanzoni mwa msimu

3. Ujio wa Tshishimbi , Banka

Simba imekuwa ikifanikiwa kwenye michezo mingi kutokana na kuweza kutawala safu ya kiungo. Hata hivyo ujio wa Mohammed Issa 'Banka' na kupona kwa Papi Tshishimbi kumeongeza ushindani wa safu ya kiungo ya Yanga

Banka ambaye alianza kuichezea Yanga mchezo uliopita dhidi ya JKT Tanzania baada ya kumaliza adhabu yake, ameonyesha yuko tayari kwa mikikimikiki ya mchezo huo

Aidhi Tshishimbi alikuwa majeruhi kwa muda mrefu. Lakini kiwango alichoonyesha kwenye mchezo uliopita, kimempa Zahera sababu ya kumtumia kwenye mchezo huo. Tshishimbi ni kawaida yake kung'ara katika 'game' kubwa

4. Makambo, Tambwe wapo

Heritier Makambo ndiye kinara wa upachikaji mabao katika ligi kuu ya Tanzania Bara akiwa na mabao 11.

Alikosa mchezo uliopita akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano. Safu ya ulinzi ya Simba pamoja na mlinda lango Aishi Manula wameonyesha madhaifu mengi katika michezo ya hivi karibuni. Watakuwa na bahati kama Makambo hatawapeleka nyavuni

Amissi Tambwe yeye anafahamika, mchezo dhidi ya Simba ndio mchezo wake wa kujidai. Anaweza asifanye vizuri kwenye michezo kadhaa lakini unapokuja mchezo dhidi ya Simba huwa hafanyi makosa. Kwa sasa yuko timamu kiafya kuliko alivyokuwa mwanzoni mwa msimu

Simba wanaweza kudhani ushindi dhidi ya Al Ahly unawapa haki ya kushinda mchezo wa Jumamosi. Waweke akiba ya maneno kwani kitakachotokea siku hiyo hawataamini

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
17h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
21h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
22h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
22h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
2d ago
READ MORE β†’