Hatma ya Ninja kusubiri Kamati ya Nidhamu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Feb 2019
Hatma ya Ninja kusubiri Kamati ya Nidhamu

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema licha ya kushindwa kuhudhuria kikao cha Kamati ya saa 72, beki Abdallah Shaibu 'Ninja' anaruhusiwa kuitumikia Yanga hadi pale Kamati ya Nidhamu ya TFF itakapokaa kujadili suala lake

Juzi Jumapili Februari 10 Shaibu alishindwa kuhudhuria kikao cha Kamati ya Saa 72 alikokuwa ameitwa kutoa utetezi wake baada ya kutuhumiwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union

Shaibu alishindwa kuhudhuria kikao hicho kwa kuwa alikuwa na majukumu ya kuitumikia Yanga iliyokuwa na mchezo dhidi ya JKT Tanzania

Aidha Wambura amesema tofauti na msimu uliopita, ambapo mchezaji angeweza kusimamishwa kusubiri shauri lake, msimu huu kanuni hiyo imerekebishwa na mchezaji anaweza kuendelea kuitumikia timu yake akisubiri Kamati ya Nidhamu itakapoketi

Kwa maana hiyo Ninja huenda akawepo kwenye kikosi cha Yanga kitakachoikabili Simba Jumamosi Februari 16 kama Kamati ya Nidhamu haitakuwa imekaa na kufanya maamuzi ya shauri lake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’