Bodi ya ligi yaahidi viporo kumalizika kabla ya mzunguuko wa 30

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Feb 2019
Bodi ya ligi yaahidi viporo kumalizika kabla ya mzunguuko wa 30

Bodi ya ligi ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limeahidi timu zote zitakuwa na michezo sawa kuanzia raundi ya 30

Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura amesema licha ya kukabiliwa na changamoto upangaji wa ratiba kutokana na muingiliano wa michuano mbalimbali, amesema watahakikisha michezo yote ya viporo inakamilika kabla ya kuanza kwa raundi ya 30

Wakati baadhi ya timu zikiwa zimecheza michezo 26, nyingine zina mechi 22, 23, 24 na 25 huku Simba ikivunja rekodi kwa kuwa na viporo 11 ikiwa imeshuka dimbani mara 15 tu

Wambura amesema ligi itamalizika mwezi Mei kama ilivyopangwa

Kumekuwa na mjadala kuhusu ubora wa ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu kutokana na sintofahamu ya ratiba huku ligi hiyo ikiwa haina mdhamini

Aidha, idadi kubwa ya viporo kwa Simba imeibua maswali mengi kutoka kwa wadau, baadhi wakiwa na hofu ya kuandaliwa kwa mazingira ya kuisaidia timu hiyo kutetea ubingwa iliyotwaa msimu uliopita

Lakini hapana shaka kama Bodi ya ligi itahakikisha viporo vyote vinamalizika kabla ya kuanza kwa raundi ya 30, angalau itarejesha ushindani uliosawa baina ya timu zinazowania ubingwa na hata zile zinazopigania kubaki ligi kuu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’