Beki Kayembe Kanku Fiston ametua jijini Dar es salaam kufanya majaribio kwenye klabu ya Yanga ambapo akifuzu atasajiliwa katika dirisha dogo la usajili mwezi wa 11.
Kayembe anatokea klabu ya SM Sanga Balende yenye makazi yake Jiji la Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kiungo Papi Kabamba Tshishimbi ndiye aliyependekeza jina la beki huyo ambaye mwenyewe amemuita mtu wa kazi.
Yanga itashiriki michuano ya klabu bingwa Afrika msimu huu hivyo kuna ulazima wa kuwa na kikosi imara hasa hasa kuimarisha safu ya ulinzi ambayo imeonekana kuwa na mapungufu.
Ili kuanza majaribio yake, Kayembe atamsubiri kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina ambaye amepata msiba na kurejea kwao nchini Zambia.
Lwandamina anatarajiwa kurejea Jumapili ijayo.

ADVERTISE HERE