FT : JKT Tanzania 0-1 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Feb 2019
FT : JKT Tanzania 0-1 Yanga

Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga wameendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuichapa JKT Tanzania bao 1-0 katika mchezo uliopigwa dimba la Mkwakwani mkoani Tanga

Bao pekee la Yanga katika mchezo huo lilifungwa na Feisal Salum 'Fei Toto' kwenye dakika ya 26 akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Gadiel Michael

Gadiel aliambaa na mpira wingi ya kushoto kabla ya kumimina majaro ya chinichini iliyokutana na mguu wa Fei Toto

Mchezo huo haukuwa mwepesi kwani JKT Tanzania ilitoa upinzani mkali lakini ushindi kwa Yanga ndio matokeo muhimu zaidi

Yanga imezidi kujichimbia kileleni baada ya kufikisha alama 58

Aidha leo kwa mara ya kwanza kiungo Mohammed Issa 'Banka' aliitumikia Yanga akiingia kuchukua nafasi ya Mrisho Ngasa kwenye kipindi cha pili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’