Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Yanga leo wanashuka katika dimba la Mkwakwani kuikabili JKT Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara raundi ya 25
Yanga iko jijini Tanga tangu juzi ikirejea mkoani humo kwa mara ya pili katika kipindi cha wiki moja
Februari 03 ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Coastal Union katika mchezo uliopigwa dimba la Mkwakwani
Baada ya mchezo huo Yanga ilielekea mkoani Singida ambapo februari 06 ililazimishwa suluhu ya bila kufungana na Singida United
Baada ya kushindwa kupata ushindi katika michezo mitatu iliyopita, mchezo wa leo una umuhimu wa kipekee kwa mabingwa hao wa kihistoria kupata ushindi
Ushindi katika mchezo huo utakiweka kikosi cha Mwinyi Zahera katika hali nzuri kuelekea mchezo wa watani wa jadi utakaopigwa Jumamosi ijayo katika uwanja wa Taifa
Yanga leo itashuka dimbani bila kinara wake wa mabao Heritier Makambo ambaye atakosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano
Hata hivyo Amissi Tambwe huenda akarejea kikosini baada ya kupona majeraha
Katika mchezo huo pia huenda Yanga ikamtumia kiungo wake Mohammed Issa 'Banka' aliyemaliza adhabu ya kufungiwa miezi 14
Jana Yanga ilithibitisha kuipokea leseni ya kiungo huyo aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar