Uongozi wa Yanga ulilazimika kumrejesha jijini Dar es salaam kiungo wake fundi Thabani Kamusoko baada ya kuumia katika mazoezi kuelekea mchezo wa leo dhidi ya JKT Tanzania
Kamusoko alichanika nyama za paja na baada ya kurejea Dar alifanyiwa uchunguzi zaidi wa jeraha lake kubaini ameumia kwa kiasi gani
Viongozi wa Yanga wanafanya jitihada kuhakikisha kiungo huyo anatibiwa haraka ili aweze kuuwahi mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi ijayo kwenye dimba la Taifa
Hata hivyo upo uwezekano mdogo wa kiungo huyo kuuwahi mchezo huo
Katika michezo ya hivi karibuni Kamusoko alionyesha kurejea kwenye ubora wake baada ya kupona majeraha yaliyomuweka nje muda mrefu msimu uliopita
ADVERTISE HERE