Yanga imepata pigo baada ya kiungo wake fundi Thabani Kamusoko kuumia mazoezini jana mkoani Tanga
Kamusoko alipata majeraha ya kuchanika nyama za paja katika mazoezi ya Yanga yaliyofanyika katika uwanja wa shule ya Sekondari ya Popatlal
Kiungo huyo amerejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya matibabu zaidi
Kamusoko ameungana na beki Abdallah Shaibu 'Ninja' kukosa mchezo wa kesho sambamba na mshambuliaji kinara wa mabao Heritier Makambo ambaye ana kadi tatu za njano
ADVERTISE HERE