Kiungo Mohammed Issa 'Banka' atakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoikabili JKT Tanzania kesho kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara utakaopigwa dimba la Mkwakwani baada ya kupata leseni kutoka TFF
Uongozi wa klabu ya Yanga umethibitisha kupokea leseni ya Banka hivyo kumfanya awe na sifa ya kushiriki michezo ya ligi na kombe la FA
"Leseni ya kiungo Mohamed Issa Juma 'Banka' tayari imetumwa kwetu na shirikisho la soka nchini, hii ina maana kuwa Banka yuko huru kucheza mchezo wa kesho dhidi ya JKT Tanzania endapo benchi la ufundi wataona inafaa kumtumia kulingana na mazoezi aliyokwishafanya," imesema taarifa ya Yanga
ADVERTISE HERE