Yanga yazipigia hesabu pointi tatu za JKT Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Feb 2019
Yanga yazipigia hesabu pointi tatu za JKT Tanzania

Vinara wa ligi kuu ya Tanzania Bara Yanga wameacha alama saba kati ya tisa katika michezo mitatu iliyopita

Baada ya kufungwa na Stand United bao 1-0, Yanga ililazimishwa sare katika michezo miwili iliyopita dhidi ya Coastal Union na Singida United

Kesho Yanga inashuka tena katika dimba la Mkwakwani kuikabili JKT Tanzania katika mchezo mwingine unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali

Ni mchezo ambao Yanga inahitaji kushinda ili isivuruge zaidi mipango yake ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu

Nahodha wa Yanga Ibrahim Ajib amesema wachezaji wote wanatambua umuhimu wa alama tatu kwenye mchezo huo na watahakikisha wanapata matokeo mazuri

Ajib amewataka mashabiki wa timu hiyo wasikate tamaa kwa kuwa bado ni mapema sana kuiondoa timu hiyo kwenye mbio za ubingwa

"Kwanza kitu cha kushangaza ni kuona tunakatishwa tamaa kwa kupoteza mchezo mmoja na kutoka sare michezo miwili, haya ni matokeo ya kawaida katika soka ila ubingwa bado upo wazi tunawaomba wanachama watuunge mkono na kutawapa ile raha waliyozoea," amesema Ajib

"Hata sisi tunaumizwa na kinachotokea kikubwa tunamshukuru Mungu kwa kuambulia pointi mbili katika mchezo wa Coastal na Singida tunaamini bado tuna safari ngumu kuhakikisha tunafikia malengo tuliyojipangia"

Baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania kesho, kikosi cha Yanga kitarejea jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi ijayo, Februari 16 2019

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’