Usiache kuchangia, mchango wako ndio utaleta wachezaji wazuri

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Feb 2019
Usiache kuchangia, mchango wako ndio utaleta wachezaji wazuri

Tangu kuondoka kwa aliyekuwa Mwenyekiti na Mdhamini wa Yanga Yusufu Manji, mambo yameyumba Jangwani.

Athari zimekuwa kubwa zaidi kwa kuwa timu haikuwa na mpango mbadala, ilikuwa tegemezi kwa Manji kwa asilimia 100

Naamini magumu inayopitia Yanga sasa limekuwa funzo zuri kwao na hata kwa timu nyingine ambazo bado zinatumia mfumo wa kutegemea mfuko wa mtu mmoja

Msimu uliopita Yanga ilishindwa kufanya usajili mzuri kutokana na ukweli kwamba HAIKUWA NA FEDHA.

Hata msimu huu Yanga imeshindwa kuwasajili wachezaji iliyowataka hasa katika usajili wa dirisha dogo kwa kuwa HAIKUWA NA FEDHA.

Mashabiki wamewalalamikia viongozi wao kwa kumkwamisha kocha Mwinyi Zahera baada ya kushindwa kuwasajili wachezaji aliokuwa amewapendekeza.

Lakini ukweli ni uleule kilichopelekea mipango hiyo ikakwama ni kwa sababu Yanga HAIKUWA NA FEDHA

Kocha Mwinyi Zahera amebaini changamoto hiyo na sasa ameamua kuchukua hatua kwa kuwashirikisha Wana Yanga ambao kimsingi ndio wenye timu

Ameweka wazi mipango yake ya msimu ujao kuwa ni kusajili wachezaji wazuri wenye hadhi na watakaoipa Yanga mafanikio makubwa.

Sasa badala ya Wana Jangwani kulalamika tena kuwa mchezaji fulani ameshindwa kusajiliwa kwa sababu ya ukosefu wa fedha, ni wao watakaotoa fedha za usajili

Kwa umoja na wingi wao, jambo hili linawezekana na kwa kuchangia angalau Tsh 2,500/- tu kwa mwezi, mipango hiyo itakamilika

Pamoja na mambo mengine, fedha hizi ambazo Wana Jangwani wanahimizwa wachangie, zitatumika kusajili na kulipa mishahara ya wachezaji

Kama timu itashindwa kusajili wachezaji wazuri msimu ujao, lawama hazitakuwa za viongozi pekee, bali zitakuwa kwa Wana Jangwani wote kama watashindwa kutimiza wajibu wao

Alichofanya Zahera ni kuweka utaratibu mzuri ambao utahakikisha fedha zinazochangishwa zinakuwa salama

Hivyo zoezi hili linaloendelezwa sasa ni mhimu na ni vyema kila mmoja wetu akaendelea kuchangia kadiri anavyoweza ili kuhakikisha malengo ya timu yanafanikiwa

Naamini hiki ni kipindi cha mpito, timu ikishapata uongozi kamili utaratibu mzuri zaidi wa kuiendesha Yanga utapatikana

Tukumbuke, ni jukumu la kila mmoja wetu kuichangia timu sasa ili baadae tusilalamike kuwa tumeshindwa kufanya usajili wa maana..

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’